Kuhusu JWT
Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania ni Taasisi iliyosajiliwa kisheria
chini ya sheria ya Societies Act, Cap,337 RE2002 ya mwaka 1954, Malengo
makuu ya kuanzishwa kwa Jumuiya hii ni pamoja na kuwaunganisha kwa
pamoja
Wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika eneo la Tanzania Bara ili kuwawezesha kutoa mawazo na maoni yao
kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara kwa
nia ya kuyawasilisha kwenye mamlaka mbalimbali ndani ya serikali.
Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania
imekuwa ikishirikiana na Serikali katika kutengeneza mazingira bora ya uanzushwaji wa biashara na kukuza uchumi wa watanzania na Taifa.
Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania JWT ni chombo cha wafanyabiashara kujiunga ili kuweza kupata huduma mbalimbali zilizo tajwa kwenye katiba ya Jumuiya na Matamko mbalimbali ya Vikao vya Jumuiya yetu.
Jumuiya katika kutekeleza majukumu yake ina mfumo wa kujiendesha kiofisi kuanzia ngazi za Maeneo Maalumu ya Kibiashara , Wilaya ,Mikoa na Ngazi ya Taifa
Wajibu wa ofisi za Jumuiya umo ndani ya katiba ya Jumuiya yetu na kila mmoja anahudumiwa bila Upendeleo wa namna yeyote
Dira ya Jumuiya
Kuwezesha kuwa na wafanyabiashara waliohamasika kwa kiwango cha juu kuweza kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya biashara ili kuboresha shughuli hizi na kuziweka kuwa kipaumbele katika maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kwa manufaa ya Wanajumuiya na Nchi yetu Tanzania kwa ujumla.
Dhamira
Kujenga mazingira kwa ajili ya shughuli za biashara yatakayokuwa na uwezo wa kuwawezesha Wafanyabiashara kuongeza fursa za kujiendeleza na kuendeleza Taifa kwa kutumia fursa zilizopo ndani na nje ya nchi