Uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania- JWT unayo furaha kubwa kutambulisha kwenu fursa mpya baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano na Benki ya CRDB PLC. Mkataba huu umelenga kuwasaidia Wafanyabiashara wote wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya Nchi.
Mkopo huu utakuwa na mashariti nafuu kwa Wanachama wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania - JWT. Ambapo sifa kuu za kuwa mnufaika ni kuwa;-
- Mwanachama wa JWT.
- Akaunti na CRDB PLC.
- Mfanyabiashara mwenye uzoefu usiopungua mwaka mmoja katika biashara husika.
- Mfanyabiashara unaeagiza mizigo kutoka nchi za nje.
- Kutumia mawakala wa forodha waliosajiriwa na TAFFA.
- Malipo yote yatafanyika moja kwa moja kwenye Mamlaka ya Bandari na TRA.
Hivyo JWT inatoa wito kwa Wafanyabiashara wa Kariakoo kwa kuanzia ambao ni waagizaji wa bidhaa kutoka nje, ambao watakuwa wamekwama fedha za ushuru wa forodha, kodi na gharama mbalimbali zinazohusiana na uingizaji wa mizigo kutoka nje kuanza kuitumia fursa hii mapema iwezekanavyo.
JWT na CRDB tumeingia makubaliano haya ili wafanyabiashara wenye vigezo na masharti yaliyowekwa, waweze kupewa mkopo huu ndani ya siku 7 (Saba) kwa kuwa mkopo huu wa dharula hautahitaji dhamana iwapo utakuwa umetimiza masharti yaliyotajwa hapo juu.
Uongozi wa JWT unatoa wito kwa wafanyabiashara wote kutumia nafasi hii kuweza kujiunga na JuAnchormuiya ili muweze kuwa wanufaika wa huduma hii adhimu kupitia Matawi ya JWT kote Nchini. Kariakoo Ofisi za Jumuiya Tawi la Kariakoo zipo Mtaa wa Mkunguni na Kongo Mkabala na Bigbon au Fika Makao Makuu ya JWT kwenye makutano ya Mtaa wa Amani na Nyamwezi, Mkabala na Msikiti wa Makonde.
Umoja wetu ndio nguvu yetu
Kwa pamojaTunaweza
Imetolewa na,
Stephen Chamle
Mkurugenzi wa Habari na Mwasiliano Taifa - JWT.
LEO 11 JUNI 2022
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania JWT Ndugu Khamis Livembe na ujumbe wake amekuwa na kikao baina ya JWT na Chama cha Wahasibu Tanzania TAA.
Kikao hiki kililenga mambo Makubwa Mawili;-
- Kufahamiana
- Kuangalia namna ya Kushirikiana
Majadiliano haya yamekuwa yenye Mafanikio makubwa ambapo kwa pamoja JWT na TAA tumekubaliana tutashirikiana katika maeneo tuliyo yabainisha hasa ya kutoa elimu kwa Wafanyabiashara kujua haki zao za kihasibu pia Kuainisha Wahasibu wanaokidhi vigezo.
Jumuiya ilipokea Mwaliko wa TAA kwa mikono miwili na tunatarajia kama Jumuiya kuingia makubaliano Rasmi ya kushirikiana ambayo yatakapo andaliwa yatatangazwa.
Tunawashukuru TAA kwa utayari na moyo wa mashirikiano Jumuiya inaahidi kuwa mshirika wa kweli katika kusaidia Wafanyabiashara na Taifa kwa ujumla
Kwa pamoja Tunaweza
Imetolewa na Idara ya Habari na mawasiliano Taifa
Uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania JWT, unapenda kuwakaribisha Viongozi wote wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania kutoka Nchi nzima kuhudhuria Mkutano Mkuu wa JWT utakaofanyika tarehe 16 na 17 Novemba 2022, Nefaland Hotel_Manzese jijini Dar es salaam.
Hivyo kutokana na unyeti wa Mkutano huu tunaomba Wajumbe husika wote wenye sifa ya Mkutano huu tusipange kukosa kwa umuhimu wake na mustakabali wa biashara zetu nchini kwa maana ya
i)BODI YA WADHAMINI
ii)BODI YA UONGOZI
iii)SEKRETARIETI TAIFA
iv)SEKRETARIETI ZA KILA KANDA NA MKOA
v)MWENYEKITI NA KATIBU WA KILA WILAYA