TAARIFA KWA VIONGOZI NA WAFANYABIASHARA WOTE NCHINI

LEO 11 JUNI 2022
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania JWT  Ndugu Khamis Livembe na ujumbe wake amekuwa na kikao baina ya JWT na Chama cha Wahasibu Tanzania TAA.

Kikao hiki kililenga mambo Makubwa Mawili;-

  1. Kufahamiana
  2. Kuangalia namna ya Kushirikiana

Majadiliano haya yamekuwa yenye Mafanikio makubwa ambapo kwa pamoja JWT na TAA tumekubaliana tutashirikiana katika maeneo tuliyo yabainisha hasa ya kutoa elimu kwa Wafanyabiashara kujua haki zao za kihasibu pia Kuainisha Wahasibu wanaokidhi vigezo.

Jumuiya ilipokea Mwaliko wa TAA  kwa mikono miwili na tunatarajia kama Jumuiya kuingia makubaliano Rasmi ya kushirikiana ambayo yatakapo andaliwa yatatangazwa.

Tunawashukuru TAA kwa utayari na moyo wa mashirikiano Jumuiya inaahidi kuwa mshirika wa kweli katika kusaidia Wafanyabiashara na Taifa kwa ujumla
Kwa pamoja Tunaweza

Imetolewa na Idara ya Habari na mawasiliano Taifa

LIVE | ADHUHURI LIVE - AZAM TV Changamoto za Wafanyabiashara

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Adallah Mwinyi akifanya mahojiano ya moja kwa moja na Mwandishi wa Azam TV kwenye kipindi cha ADHUHURI LIVE - AZAM TV 26/11/2020